Header Ads

HALMASHAURI YATIKWA TUHUMA ZA KUTOKUWALIPA WAFANYAKAZI MADENI.


Halmashauri ya wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga inatuhumiwa kutokuwalipa fidia ya mishahara wafanyakazi wa kiwanda cha Mnazi kilichopo kijiji cha kwemkwazu kata ya Mnazi   kutokana  na aliyekuwa mwekezaji wa kiwanda hicho  kunyang’anywa na serikali kwa kushindwa kukiendeleza kwa muda wa miaka 15. 

Wafanyakazi hao wametoka kilio hicho leo kiwandani hapo baada ya Ziara ya  Mbunge wa Jimbo la Mlalo  Rashid Shangazi   alipowatembelea  kwa lengo la kutaka kufahamu changamoto zinazowakabili wafanyakazi hao.

Akizungumza kwa niaba ya Wafanyakazi wengine  wa kiwanda cha Mnazi Martin Lyimo amesema wao walikuwa waajiri kabla ya kiwanda kufungwa na baada ya mwekezaji huyo kunyang’anywa na serikali hawakupewa  barua ya kusimamishwa kazi hivyo  wanahaki ya kudai haki yao .
Mfanyakazi Abas Ulanga ameiomba serikali kuingilia kati sakata hilo ili Mwekezaji huyo aweze kuwapatia haki zao na kuongeza kuwa kama malipo yao hayatalipwa wataandamana.
Akijibu tuhuma hizo Mbunge wa jimbo hilo Shangazi amesema pesa zipo isipokuwa  Utaratibu bado unafanyika ili wafanyakazi hao waweze kupatiwa fedha zao vizuri na kwa utaratibu unaofaa.
Mbali na hayo Mbunge huyo ametoa rai kwa wafanyakazi hao pamoja na kupatika kwa riziki ambayo itawasaidia kujikimu katika mahitaji yao lakini jambo la msingi kufungua mashamba ya mkonge ambayo yatawasaidia kuwaongezea kipato.
Akiendelea kuwatoa hofu wafanyakazi hao Diwani  kata ya Mnazi  Zuberi Chachambo amesema kwa mujibu wa utaratibu wa serikali  baada ya kuuza shamba hilo kwa mwekezaji mwingine kuna mkataba ambao lazima usaini na mwanasheria mkuu wa serikali hivyo  pesa zao zitalipwa baada ya tukio hilo kufanyika.
Awali Shamba la mnazi huo lilikuwa linamilikiwa  na kampuni ya Limansi ambapo mkurungezi wake aitwaye Laurent Machalia ndiye anayetuhumiwa  kuzoefisha kiwanda hicho kwa muda mrefu na matokeo yake kuporwa na serikali kwa mujibu wa sheria hadi sasa kiwanda hicho kinamilikiwa na mwekezaji mwingine na  changamoto kwa sasa haipo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.