Header Ads

Hivi Ndivo Daimond Alivyovuruga Ndoa ya Zari na Maulid Kitenge
Imevuja! Baada ya hivi karibuni picha mbalimbali zikimuonesha Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha EFM, Maulid Kitenge akijiachia nyumbani kwa mjasiriamali maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ huko Afrika Kusini ‘Sauz’ na kufunguka kuwa ana mpango wa kumuoa, mpango huo umetibuka.

Aliyeutibua ni mzazi mwenzake na mwanamama huyo msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye amedaiwa kumzidi nguvu akinomanoma mtangazaji huyo.

Chanzo makini kutoka Sauz kilieleza kuwa Kitenge alikuwa kwenye maandalizi ya kupeleka posa ili atimize alichomuahidi Zari, lakini mipango hiyo imeingia dosari, tulia ujuzwe zaidi.

“Unajua Kitenge alikuwa kwenye maandalizi na kwamba hivi karibuni posa ilikuwa ipelekwe na mipango ya ndoa ifanywe lakini upepo umegeuka baada ya Diamond kuonekana kupedwa zaidi na watu wa karibu na Zari wakiwemo mashabiki wa  mwanamama huyo ambaye ni raia wa Uganda,” kilisema chanzo hicho.

DIAMOND AMETIBUAJE?

Chanzo kiliendelea kutiririka kuwa Diamond anatajwa kutibua ndoa hiyo ya mama watoto wake na Kitenge kwa kuwa Waganda wanampenda sana na wanatamani yeye ndiyo amuoe Zari lakini siyo mwanaume mwingine yeyote.

“Huko Uganda ambapo ndipo alikozaliwa Zari, Diamond bado ana nafasi kubwa sana kwani anakubalika mno na jamii, kwa hiyo hawamtaki huyo Kitenge kabisa hali ambayo pia imemweka Zari njia panda,” kilitiririka chanzo.

WAGANDA WACHARUKA

Habari ziliendelea kuelezwa kuwa Waganda wamecharuka vilivyo baada ya kusikia Kitenge anataka kumuoa Zari jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia kwani wao wanayemfahamu na kumkubali zaidi ni Diamond na siyo mwingine.

“Kumekuwa na maneno mengi sana kwenye mitandao ya kijamii, lakini kikubwa ni ishu ya zari kuolewa na Kitenge, wengi wamesema kuwa hawamshauri Zari asifanye hivyo na endapo atalazimisha wametishia kutomuunga mkono kwenye shughuli zake za biashara.” kilisema chanzo.

Msimamo huo wa mashabiki wake unatajwa kuwa umemtikisa mwanamama huyo kiasi cha kutojua nini cha kufanya ambapo chanzo cha karibu na Zari kimeliambia Amani kwamba The Boss Lady hana mpango wa kufunga ndoa na Kitenge.

KITENGE ANASEMAJE?

Ili kuujua ukweli juu ya suala la kukataliwa kwake ukweni, Amani lilimtafuta Kitenge ambaye alisema hajali chochote na mipango yake ya kumposa Zari iko palepale.

“Hao wanaosema maneno hayo kwamba nimekataliwa hivyo mpango wa kumposa Zari umeishia hapo ni waongo, ninachosema mimi ni kwamba niko kwenye mipango ya kupeleka posa muda wowote,” alisema Kitenge.

VIPI UPANDE WA DIAMOND?

Katika kuleta usawa wa habari gazeti hili lilimtafuta Diamond ili aeleze anazungumziaje suala hilo, simu yake ya mkononi haikuwa hewani.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.