Header Ads

IDARA ya uhamiaji Dodoma yatoa pasipoti 409


IDARA ya uhamiaji Mkoani Dodoma imetoa jumla  ya pasipoti 409 za mfumo wa kimtandao (E-PASIPOTI)  kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma tangu kuzinduliwa kwa mfumo huo hali inayotajwa kuleta matumaini makubwa katika zoezi hilo.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na  Afisa uhamiaji Mkoa wa Dodoma PETER KUNDY ,kwamba mwitikio umekuwa mkubwa tangu kuzinduliwa kwa mfumo huo mwezi Aprili mwaka huu jijini hapa.

 Pamoja na hayo ameeleza kuwa paspoti hizo zimetolewa kwa watu waliokidhi masharti ya uraia wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuhusisha vyeti vya kuzaliwa vya mhusika ,vyeti vya kuzaliwa vya wazazi ,vielelezo vya shule ,udereva na barua za utambulisho wa waombaji kutoka kwa uongozi wa kata.Aidha ,pamoja na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika zoezi hilo,afisa uhamiaji huyo amesema kuwa zoezi la usajili wa paspoti hizo za kielekroniki linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  baadhi ya waombaji kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa na uraia.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.