Header Ads

INALLY: Justin Bieber amtaja mpenzi wake, mbioni kufunga ndoa

Hatimaye  Justin Bieber aweka wazi mahusiano yake yakimapenzi na mwanamitindo Hailey Baldwin hii ni baada ya tetesi kusambaa kuhusiana na wawili hao kuvalishana pete ya uchumba July 7,2018 katika visiwa vya Bahamas.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Justin Bieber ameandika ujumbe mzito baada ya kupost picha akiwa na mpenzi wake Hailey na kusema kuwa anampenda sana mpenzi wake na hatamani kushiriki hisia hizo na mtu mwingine yeyote na kukiri kumvalisha pete ya uchumba.
“Nilikuwa nataka kusubiri kidogo lakini maneno yanasambaa sana , nakupenda sana Hailey kutokana na kila kitu ulichonacho, nakuahidi kuiongoza familia yetu katika maadili na Mungu atulinde katika maamuzi tunayoyafanya, moyo wangu ni wako daima na utakuwa wa kwanza katika kila kitu”
“Wewe ndio  kipenzi cha maisha yangu na sitaki ku’share hisia hizi na mtu mwingine unanifanya nijisikie vizuri na tunakamilishana , siwezi kusubiri msimu wa maisha yetu , inafurahisha kwasababu kila kitu sasa hivi kinaleta maana , kitu ambacho kinanifurahisha zaidi ni kuwa wadogo zangu wataona ndoa yenye malengo na watajifunza kitu kupitia hapa”
“Muda alioupanga Mungu siku zote ni sahihi , nilikuvalisha pete siku ya sabasaba , kiimani namba ya saba huwa ni nzuri, lakini sikupanga hili litokee nafurahi kuona maisha yetu ya mbeleni yapo salama, kwa yule aliyepata mke basi amepata kitu kizuri na neema kutoka kwa Mungu”

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.