Header Ads

JAFO AWAPONGEZA WILAYA YA MANYONI KWA UJENZI MZURI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa wilaya ya Manyoni kwa kusimamia vyema fedha za serikali zilizowezesha kujenga vizuri sana kituo cha afya Kitinku.
Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayo tekelezwa chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI. 
Jafo ameridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya Kitinku ambacho serikali  ilipeleka shilingi milioni 500 ili kufanya uboreshaji na kujenga majengo mbalimbali ikiwemo jengo la huduma za upasuaji.  
"Niwapongeze viongozi wote kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo hiki ambacho ni mfano wa kuigwa kwa vituo vingine,"alisema Jafo.
Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Mhe . Daniel Mtuka pamoja na Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi  Miraji Mtaturu kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuiunganisha timu ya watendaji na wanajamii wa Manyoni.
Kwa upande wake mh Mtaturu amemshukuru waziri Jafo kwa  maelekezo na ushauri wake mbalimbali anaoutoa uliowezesha kufikia hatua hiyo ya uboreshwaji.
"Mheshimiwa waziri pamoja na pongezi zangu kwako, nikuombe utupelekee salaam za shukrani kwa mhe Rais kwa kutuletea pesa za maendeleo mbalimbali,"alisema mh Mtaturu.
Ameshukuru pia kwa gari ya wagonjwa waliyopatiwa na watumisho wa afya 47 waliopelekwa wilayani humo na kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha kituo cha afya Nkonko.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.