Header Ads

jeshi la polisi mkoa wa morogoro lafanya oparesheni kwa magari yaendayo mikoani
KUFUATIA  operasheni  za mara kwa mara  zinazofanywa na  jeshi la polisi   mkoani Morogoro  kwa magari  yaendayo mikoani   zimeanza kuleta matokeo  chanya baada ya  leseni  4,734  kukaguliwa na  huku madereva  tisa wakifikishwa  mahakamani , kati yao watano  wamehukumiwa kifungo cha miezi minne jela na faini ya shilingi elfu kumi .

Akizungumza   mara baada ya kukagua magari yaendayo mikoani katika kituo Kikuu cha mabasi  Msamvu mjini Morogoro kamanda wa polisi  mkoanihumo  Wilbrod Mutafungwa  amesema  zoezi hilo la  ukaguzi  magari ni endelevu  na kwamba  wamewafikisha mahakamani  Madereva hao  tisa na kuchukuliwa hatua   ili iwe fundisho kwa madereva wengine wanaokiuka sheria


Pia kamanda Mutafungwa amewatahadharisha abiria  wenye tabia ya kuwashawishi na kushabikia dereva kuendesha mwendo kasi kuacha tabia hiyo kwani zoezi hilo ni muhimu  na kwamba linalenga kuokoa maisha  ya abiria.


Kwa upande wao  mmoja wa madereva wa mabasi Bw. Hashim Mohamedi  na  Bi PJamila Peter wamelishukulu jeshi la  polisi kwa hatua hiyo na kushauri  zoezi hilo kuwa  enderevu  na kuomba kuzingatia muda ili kuepusha usumbufu kwa abiria.
    

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.