Header Ads

Kesi ya BILIONI 300 ya Rugemalira na Seth imeahirishwa tena leo

Leo July 5, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mmiliki wa IPTL, Harbinder Seth na mwenzake hadi July 19,2018kwa sababu upelelezi haujakamilika.
Wakili wa serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kwamba shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.
Hata hivyo, wakili wa utetezi Hajra Mungulla aliuomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi July 19,2018.
Mbali na Seth mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara James Rugemalira ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 300.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.