Header Ads

kituo cha east afrika redio chapongezwa

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP), Abdul Nondo amekipongeza kituo cha habari cha  East Africa Radio kuwa mstari wa mbele katika kufuatilia suala la changamoto ya usajili wa kuomba mkopo  iliyokuwa inawakumba wanafunzi wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu  mwaka 2018.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP), Abdul Nondo, Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo Abdul –Razaq Badru
Nondo ametoa pongezi hizo ikiwa ni masaa machache baada ya bodi ya mikopo kutangaza kusogeza mbele muda wa kusajiliwa kuomba mikopo, ambapo awali ilitakiwa iwe mwisho Julai 15, na kupeleka muda mbele hadi mwisho wa mwezi huu.
Kupitia kipindi cha East Africa Breakfast kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kilifanya mazungumzo na Bodi ya Mikopo pamoja Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA)  pamoja na wanafunzi wanaotaraji kuomba mkopo, kuhusiana na changamoto ya muda katika kuhakiki vyeti vya kuzaliwa vya wanafunzi hao ambapo waliahidi kukaa kwa pamoja na kufanyia kazi changamoto hizo.
"Tunashukuru sana East Africa Radio katika uufuatiliaji wa kina kuhusu suala hili la bodi ya mikopo, mmelisemea sana . Tunaishukuru pia bodi kwa kuweza kusogeza muda mbele. Ni jambo jema, tunaishukuru bodi kusikiliza kilio cha wanafunzi" Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi, Abdul Nondo.
Changamoto ambazo zilikuwa zikilalamikiwa na wanafunzi ni pamoja na RITA kuchukua muda mrefu katika kuhakiki vyeti huku muda uliowekwa na bodi ya mikopo katika kusajili ukiwa haulingani na idadi ya wanafunzi waliotuma maombi.
Licha ya changamoto ya muda, RITA wamekuwa wakilalamikiwa kufanya shughuli zao kwa taratibu, hivyo Mtandao huo wa Wanafunzi wameahidi kuwaandikia barua ili waweze kwenda sambamba na bodi ya mikopo ili changamoto tajwa ziweze kukamilika na wanafunzi wanaostahili kupata mikopo waweze kupatiwa ili kuepusha usumbufu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.