Header Ads

Ligi daraja la kwanza kuchezwa kwa staili mpya

Katika juhudi za TFF kuboresha ushindani kwenye ligi kuu, ligi daraja la kwanza na la pili nchini, kamati ya mashindano ya shirikisho hilo imepitisha mfumo mpya wa uendeshaji wa ligi dadaraja la kwanza (FDL) kuanzia msimu ujao.
Moja ya mechi za ligi daraja la kwanza msimu uliopita
Kamati hiyo imepitisha mfumo ambao utazigawa timu shiriki katika makundi mawili yenye timu 12 badala ya mfumo wa sasa ambao ulizigawa timu hizo kutokana na ukanda.
Katika mfumo huo mpya, timu itakayoongoza kundi itapanda moja kwa moja ligi kuu huku timu zitakazomaliza nafasi ya pili naya tatu katika kila kundi zikicheza mtoano kwa mechi ya nyumbani na ugenini kisha mshindi kucheza na timu zilizomaliza nafasi ya 17 na 18 katika ligi kuu ili kupata mshindi atakayepanda .
Timu hizo mbili zilizomaliza nafasi ya 17 na 18 katika ligi kuu endapo zitapoteza michezo hiyo zitaungana na timu zilizomaliza nafasi ya 19 na 20 kushuka daraja.
Pia kamati hiyo imekubaliana na mfumo wa mpya wa mashindano ya Taifa Cup ambayo yatachezwa kati ya mwezi Juni na Julai 2019 huku mashindano ya vijana ya U15 yakichezwa katika mtindo wa Copa CocaCola .
Mashindano ya U17 yenyewe yatahusisha klabu za ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili kwa pamoja kumpata mshindi mmoja na michuano ya shirikisho yakianzia katika ngazi ya mkoa ambapo kila mkoa utakuwa na bingwa wake.
 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.