Header Ads

MBARAWA ATOA MIEZI 6 KWA DUWASA KUONGEZA MAPATO

WAZIRI wa Maji Na Umwagiliaji Profesa MAKAME MBARAWA ameipa miezi sita Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) kuhakikisha inapandisha makusanyo yake kutoka bilioni 1.3 hadi kufikia shilingi Bilioni 1.8.

Akizungumza jijini Dodoma kwenye ofisi za DUWASA kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maji profesa MBARAWA amesema  katika kipindi hicho kila mtendaji atapimwa katika kutekeleza agizo hilo.

 Amesema DUWASA inafanya biashara hivyo inapaswa makusanyo yake yaongezeke ili fedha zikipatikana ziwekezwe kwenye miundombinu ya maji na kupunguza changamoto zilizopo.

 Mbali na hilo amewataka watendaji wa Mamlaka hiyo  kuwa waadilifu kwa kuhakikisha hawashirikiani na wananchi kuisababishia DUWASA hasara na badala yake wajikite kwenye uzalishaji unaotakiwa.

Awali akisoma taarifa  Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA  Mhandisi DAVID PALLANGYO amesema makusanyo Kwa Mwaka ni shilingi Bilioni 1.3 na kutaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni upotevu wa Maji Kwa asilimia 28.7 kutokana na baadhi ya watumiaji kuiba maji au kutumia maji kwa wizi.

Changamoto nyingine ni uchakavu wa mita za maji ambapo ili kukabiliana Na changamoto hiyo mhandisi PALANGYO amesema wana mpango wa kuleta mtambo mpya wa kupima ubora wa mita zilizopo.


Ametaja mikakati ya kubaliana na changamoto hizo kuwa ni pamoja na kuchimba visima vya maji kwenye njia ya kwenda Dar es Salaam na Singida na kutoa Ombi kwa Wizara kuwaruhusu kutumia bwawa la Farkwa ili kuongeza uzalishaji wa maji.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.