Header Ads

Mbunge wa Mlalo: ''Lamuhimu kuhakikisha sisi tunabaki kuwa kama ndugu''.


Wafugaji na wakulima nchini  wametakiwa kuishi kwa amani na upendo ili kujenga ushirikiano mzuri kati yao.
Hayo yamesemwa leo  na  Mbunge wa Jimbo la Mlalo Mkoani Tanga Rashid Shangazi  wakati wa ziara yake alipotembelea kukagua Josho la Kitongoji cha Kammba Kata ya Lunguza Wilaya ya Lushoto Mkaoni Tanga.

‘’Tusiishi kama Maadui ,Lakini la muhimu sana ni kuhakikisha sisi tunabaki kuwa kama ndugu , tunabaki kutumia mazingira tuliyokuwanayo kwa faida yetu, tunabaki kuzungumza lugha moja kutatua changamoto zetu tukishaanza kutengana kwamba hawa ni wakulima na hawa ni wafungaji watu watatuvuruga,’’.

Mbali na hayo ametoa rai kwa umoja wa wafugaji kukaa na uongozi wa kijiji kutafuta utaratibu mzuri ambao utasaidia kutatua changamoto ambazo zinawakabili ikiwemo uhaba wa malisho, ubovu wa miondombinu pamoja na kupunguza gharama za kuoshea mifugo.

Wakizungumzia changamoto zinazowakabili moja ya wafugaji wa kijiji cha kivingo kata ya Lunguza Wilaya ya Lushoto Merian Moreto na Baraka Yohana Mkazi wa Kjiji cha Mng’aro, kata ya Mng’aro wilaya ya Lushoto Mkoani huo  wamesema changamoto kubwa ni maeneo ya hifadhi na kuiomba serikali kuingilia kati Mgogoro unaoendelea kati yao na mahakama ya rufaa  ya Arusha   wa Hifadhi maana imekuwa ni changamoto  takribani kwa  miaka 30 na hivyo wamekuwa ni watu wa kurandaranda, kunyan’ganywa mifugo yao , kukamatwa na kutozwa mamilioni hata mifugo kufungiwa zaidi ya siku nne.


Awali akizungumza afisa Ugani Kata ya Lunguza  Mussa Mgonja  amesema wao kama halmashauri watakikishwa mwaka hauishi watakuwa wametatua changamoto ya malisho ili kuweka mipaka mizuria ambayo itawasaidia wafugaji hasa kwa kiasi kikubwa.


Ziara ya Mbunge Shangazi  ya kutembelea jimboni kwake inaendelea ambapo leo aliweza kutembelea Kijiji cha Kivingo Kata ya na kufanya mkutano wa hadhara na wanafugaji,kukagua Josho katika kkitongoji cha Kummba na kutembelea mifereji ya Scheme , kituani Mwezae Skimu na Kwengiri Skimu.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.