Header Ads

NDEJEMBI ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA FEDHA ZA SERIKALIKaimu mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya kongwa DEO NDEJEMBI amerizishwa na ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa fedha za serikali katika wilaya ya Dodoma mjini.

Akiwa katika ziara ya kutembelea miradi hiyo bw Ndejembi aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya pomoja na na wataalamu mbalimbali wa halimashauri ya jiji ili kuangalia  miradi yao inayotekelezwa kwa fedha za serikali ambayo mbio za mwenge wa uhuru utaipitia kwa kuzindua na kuweka jiwe la msingi.

Aidha, Ndejembi ameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo ambapo amesema zipo Dosari ndogondogo zimejitokeza katika miradi hiyo ambapo ametoa maelekezo kwa wataalamu kuhakikisha wanazirekebisha dosari hizo kabla ya ijumaa .Sambamba na hayo Ndejembi  amewataka wananchi wa jiji la Dodoma  kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 5/8/2018 ambapo mwenge wa uhuru utakimbizwa wilayani hapa na kuzindua na kuweka jiwe la   msingi katika miradi mbalimbali huku akiwataka wananchi kuwa wazalendo wa nchi yao na kuwaeleza umuhimu wa mwenge wa uhuru.
Hatahivyo ,Ziara hiyo imetembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa tofali JKT makutupora, barabara ya emaunce Africa Dream, Sheli ya Mapinduzi iliyopo Dodoma Makulu, kituo cha afya Makole,kiwanda cha Thamani za maofisini na Majumbani kilichopo katika chuo cha ufundi VETA , kituo cha Biashara, jengo la Maabara ya wanafunzi Dodoma Sekondari na Madarasa katika shule ya msingi Nkuhungu ambapo miradi yote inatekelezwa na serikali ya awamu ya tano.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.