Header Ads

SERIKALI YATOA AJIRA 6,180 KADA ZA AFYASERIKALI imetoa ajira mpya elfu  6180 katika Sekta ya Afya kwenye hospitali,vituo vya afya na zahanati kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)SELEMAN JAFO amesema ajira hizo zimezingatia uhaba wa watumishi wa afya katika maeneo ya vijijini kutokana na kutokuwepo Kwa wataalam wa afya hali ambayo imepelekea wahudumu wa afya kuendesha vituo vya afya.

Amesema mchakato wa maombi ulihusisha Madaktari,Wafamasia,wataalam wa maabara pamoja na matabibu ambapo jumla ya waombaji 24,891 waliwasilisha maombi yao ambapo 6180 ndio walioajiriwa kulingana na kibali cha ajira kilichotoka.
Ametoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri kuandaa mazingira kwa watumishi hao na kwa wananchi waache kuwafanyia watumishi mambo ya ajabu pindi wanapoenda kuripoti katika vituo vya kazi bali wawe kitu kimoja.
Mgawanyo huo watumishi katika serikali za mitaa umezingatia halmashauri  zenye hospitali,vituo vya afya na zahanati zilikomilika lakini zilikuwa hazifanyi kazi ipasavyo kwa kukosa watumishi,uwepo wa vituo vya afya 210 vilivyoboreshwa katika halamshauri mbalimbali ili kuziwezesha kutoa huduma zilizokusudiwa.
Pia umezingatia halmashauri zenye zahanati zinazoongozwa na wahudumu wa afya na zile zinazoongozwa na wauguzi na zenye uhaba mkubwa wa watumishi kwa mujibu wa taarifa ya mahitaji ya watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya kulingana na uzito wa kazi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.