Header Ads

TPBO yamtaka Waziri Mwakyembe

Shirikisho la ngumi za kulipwa nchini (TPBO) limeomba kukutana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ili wajadili kuhusu mgogoro wa tasnia ya ngumi hivi sasa.
Rais wa shirikisho la ngumi za kulipwa nchini (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustadhi’(kushoto) na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia).
Akizungumza na www.eatv.tv Rais wa Shirikisho hilo, Yassin Abdallah ‘Ustadh’ amesema  kuwa wanataka kukutana na Waziri ili wamueleze ukweli wa kiini cha mgogoro huo pamoja na kutafuta suluhisho kwaajili ya maslahi mapana ya mchezo wa ngumi nchini .
 Kuhusu sababu inayopelekea ukimya wao katika tasnia hiyo kwa sasa, Rais wa Shirikisho hilo, Yassin Abdallah ‘Ustadh’ alisema .
“ Sisi hatuko kimya ila tunatafakari kwanza mambo yanavyokwenda , tumeshamwandikia barua Mkurugenzi wa michezo siku chache zilizopita tukimueleza nia yetu ya kutaka kukaa nao pamoja kwasababu sisi sio tatizo, ila kuna watu wanatumia mchezo wa ngumi kwa maslahi yao binafsi “. 
TPBO imekuwa na mgogoro wa muda mrefu  na Shrikisho lingine la ngumi za kulipwa nchini ,PST kuhusu uendeshaji wa mchezo huo licha ya juhudi kubwa za kutatua mgogoro  kufanyika na wizara husika kwa kushirikiana na Baraza la Michezo Tanzania (BMT).
Kutokana na TPBO na PST kuingilia kazi ya kamati ya kuboresha Katiba ya mchezo wa ngumi nchini ikiwemo kukosoa na kuilaumu kamati hiyo, Dkt. Harrison Mwakyembe alitoa maagizo kwa msajili wa vyama vya michezo kuwaandikia barua kali ya onyo.
 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.