Header Ads

wakazi wa kijiji cha mtumba wakerwa na uharibufu unaofanywa na wafugaji
BAADHI ya wakazi wa Kijiji cha Mtumba kilichopo nje kidogo ya Jiji la Dodoma wameonyesha kukerwa na uharibifu wa barabara unaofanywa na baadhi ya wafugaji kutokana na ukaidi kwa kupitisha mifugo yao na  hivyo kuutupia lawama uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho kwamba umeshindwa  kudhibiti hali hiyo..

Licha ya hayo,mifugo hiyo inadaiwa kusababisha ubovu wa barabara kijijini hapo ambapo ni hivi karibuni  serikali imetumia gharama kubwa kuzirekebisha.
Wakizungumza Kijijini humo baadhi ya  wanakijiji wa kijiji cha Mtumba wamesema kuwa wafugaji wa eneo hilo wamekuwa ni kero kwa kuwasababishia adha pale wanapopita kutokana na kuwepo kwa mashimo na mavumbi kutokana na uharibifu huo.

Wanakijiji hao ambao ni mama TINASHA,ANNA MAZENGO  na SAIMON KAMWELA wamesema kuwa  mifugo inayopitishwa na wafugaji  hao ina uharibifu mkubwa kwenye barabra za kijiji hicho  na kusababisha kuwa kero hasa kipindi cha masika kutokana na barabara nyingi kuwa na mashimo na matope.

Hata hivyo mmoja wa wafugaji JUMA RASHIDI amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambapo yeye amedai ameachana na vitendo vya kupitisha mifugo yake katika barabara hiyo na kuwaasa wenzake kuachana na tabia hiyo.

Faith Silla  ni mwenyekiti wa kijiji cha mtumba amekiri kuwepo Kwa adha hiyo na kusema kuwa licha ya kuwatoza faini wanaokiuka taratibu lakini bado jitihada zao zimekwama.Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.