Header Ads

WAKULIMA WALIA NA SERIKALI: TUNALIMA LAKINI HAKUNA MASOKO.


MLALO TANGA: Imeelezwa  kuwa Ili kuboresha sekta ya kilimo  Serikali inatakiwa kuongeza idadi ya masoko nchini lengo  ikiwa ni kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.
Hayo yamebainishwa leo  na wakulima wa kijiji cha Kangagai  Kata ya Mwagoi  wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wakati wa ziara ya Mbunge wa Mlalo  Rashid Shangazi alipotembelea kituo cha habari na mafunzo  kwa wakulima wa kikundi cha Mwagoi, kituo cha kukusanya maziwa Uwamwa na Mradi wa ufugaji nyuki  vyote vikiwa kata ya Mwagoi wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Kaimu mwenyekiti wa kikundi  Cha Mwagoi  Tatu Kiruwa amesema changamoto kubwa inayowakabili, wanalima mazao lakini masoko yanakuwa shida na kuongeza kuwa pembejeo za kilimo bado ni tatizo kubwa hasa kwa wakulima wadogo wadogo.

Wakizungumzia suala la maziwa wananchi hao wamesema katika kituo cha kupozea maziwa kimewasaidia watu kuweza kuwasomesha watoto wao.

Akijibu Changamoto zinazowakabili wakulima wa kata ya Mwangoi ikiwemo ya Ukosefu wa Maji  na umeme Mbunge wa jimbo hilo   amesema wao kama halmashauri watahakikisha changamoto hizo zinatatuliwa,  lengo ni kuwaelekeza wananchi jinsi ya kufunga mashine ziweze kufanya kazi.

Hata hivyo ameendelea kwa kusema  Taki la Kupokerea na kupozea maziwa (Tanzu) lenye uwezo wa lita 1500   walilopewa kwa hisani ya  Tanga fresh  mahitaji bado ni makubwa kwani taki hilo linapokea lita chini ya  mia tano kwa siku.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.