Header Ads

Wanachama wa TASO Wamlalamikia Jaji Mstaafu Edward Mwesumo mwenyekiti wa wadhamini.

wanachama wa TASO (Tanzania Agriculture Society)Wanamlalamikia jaji (Mstaafu) EDWARD MWESUMO,Mwenyekiti wa wadhamini kwa kukiuka maagizo ya Mh Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi.
Aidha wananchama wanamshukuru Mh waziri wa Mambo ya ndani kwa kuwarejeshea chama chao kilichokua kimefutwa na Msajili Mei 2017.
Wanachama hao wanamlalamikia Jaji (Mstaafu) Edward Mwesumo kwa kukiuka maagizo ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi.Katika barua yake ya kurudisha chama amabayo ni 

1) Kuitisha mkutano mkuu wa chama TASO-Taifa ndani ya siku 60 ambazo zimeisha na hadi sasa hajafanya hivyo.

2) Kuonana na viongozi wa TASO-TAIFA waliochaguliwa kwa maagizo ya Mh. Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi tarehe 30/12/2017 ambao wamefutiwa ili akabidhiwe ofisi ya TASO-TAIFA aendelee na utekelezaji ya maagizo ya Mh. Waziri hadi sasa hajafanya hivyo.

3) Kufanya uchaguzi wa viongozi wa TASO-TAIFA kuziba pengo la viongozi walioondolewa kinyume chake amejiteua yeye mwenyewe kuwa mwenyekiti TASO-TAIFA na kuteua watu wengine na kuwapa nyadhifa mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya, kanda, na taifa.

Hivyo kwa kuwa Mh Waziri wa mambo ya ndani ya nchi alitoa angalizo juu ya kutozingatia maelekezo aliyoagiza kuchukuliwa hatua za kisheria, wanachama wanamtaka Jaji (Mstaafu) Edward Mwasumo (Mwenyekiti wa Wadhamini) na si mwenyekiti wa TASO-TAIFA anavyojiita sasa kufanya yafuatayo.

1) Kufuta maagizo ya Mh Waziri

2) Kufanya kazi kwa mu

jibu wa katiba ya chama ya mwaka 1993 toleo la 2009.

3) Kuacha kufanya kazi na watu wachache, mamluki na aingie ofisini.

4) Kuacha kuteua watu kushika nyadhifa mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya, kanda na taifa

5) Kuacha kufanya kazi kama chama chake au kampuni yake binafsi na afanye kazi kwa kuzingatia kanuni, taratibu, na katiba ya TASO na muunganisho wa wadhamini na taratibu zilizopo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.