Header Ads

WATAKIWA KUKATA BIMA YA AFYA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI
CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Morogoro mjini   kimewataka viongozi na wanachama kuwa mstari wa mbele kukata bima ya afya kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya.
Akizungumza na wakazi wa kata ya Tungi mjini morogoro akiwa kwenye   ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM mwenyekiti wa chama hicho manispaa hiyo Fikiri Juma amesema  lengo la serikali ni kutaka kila mtu akate bima ya afya itakayo msaidia kupata matibabu kwa uhakika.
 Mwenyekiti Juma amesema Serikali imetoa   bima ya afya kuwasaidia wananchi kupata huduma bora katika sekta ya afya huku ikitambua kuwa wananchi  wengi wanakipato kidogo ambacho hakiwezi kutosheleza kupata huduma za matibabu wanapo ugua.
Aidha Juma amehimiza baraza la maendeleo ya kata hiyo kuhakikisha wanamalizia ujenzi wa zahanati ambayo sasa ipo kwenye rinta na kuhakikisha kua jumla ya pesa zilizochangiwa na wananchi shilingi 700,000 zinapatikana.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa niaba ya Afisa mtendaji wa kata hiyo Deogratias Kizeba amesema katika  sekta ya afya wazee 218 ndiyo walikata bima ya CHF ambazo ambazo nazo zimekwisha muda wake.
Kizeba alifafanua kuwa bima za wazee hao zililipiwa na mkurugenzi wa manispaa na kwataka wanajamii kujitokeza kukata bima hizo ili wawe na uhakika wa matibabu wanapoumwa.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.