Header Ads

watu wanne wakamatwa kwa kughushi hundi za benki.Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa kughushi hundi za benki.
Akizunguzia tukio hilo hii leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam DCP- LIBERATUS SABAS amesema mnamo tarehe 24 June mwaka huu katika maeneo ya Kariakoo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa AMINI KIMARO (55) mkazi wa Manzese na wenzake watatu kwa kosa la wizi wa kughushi hundi za benki mbalimbali na kuziweka kwenye akaunti za washirika wake.
Kamanda Liberatus  Sabas alitanabaisha  kuwa watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na uhalifu huo na wamekuwa wakighushi hundi za benki tofauti tofauti na kisha kuziweka hundi hizo katika akaunti za benki ili kufanikiwa kuiba fedha walizokusudia.
' mtu mmoja anaitwa amini kimaro (55) makazi wa manzese pamoja na wenzeke watatu walikamatwa kwa tuhumaza za  kughushi hundi na hivyo kuweza kujipatia pesa zisizo halali ' alisema Sabas 

Aidha amesema sambamba na kuwashikilia watuhumiwa hao pia jeshi la polisi linashikilia gari aina ya IST Yenye namba T 819 DED iliyokuwa ikitumiwa na wahalifu hao,simu za mkononi nane,kadi za simu sita za mitandao tofauti,pamoja na Deposit Slip ya shilingi za Kitanzania milioni moja laki tisa sabini na tatu elfu mia saba na hamsini hundi ya NMB.
Mbali na tukio hilo pia jeshi la polisi limefanikwa kumkamata OMWAILIMU SOSTHENES BINYAKUSHA kwa kosa la kutapeli watalii na kuchukua kiasi cha Dola za Kimarekani elfu tano na kushindwa kuwapeleka safari walizokubaliana.
Aidha Jeshi hilo la polisi limeendelea kuonya  kuwa katu halitokubali watu kujipatia kipato kisicho halali huku likiwataka wakazi wa Dar es Salaam kujihusisha na shughuli zilizo halali.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.