Header Ads

WIZARA YA MADINI YA SAINI MIKATABA MITATU YA UJENZI WA VITUO VYA UMAHIRI NCHINI

Serikali kupitia wizara ya madini hii leo imesaini mikataba mitatu ya ujenzi wa vituo vya umahiri vitakavyojengwa na kampuni ya suma jkt ambavyo vinatajiwa kukamilika ndani ya miezi sita ambapo lengolengo la ujenzi wa vituo hivi ni kujenga uwezo kwa wachimbaji wadogo
Akizungumza katika warsha hiyo waziri wa madini angela kairuki amesema hii ni hatua ya utekelezaji wa bajeti ya wizara ya madini aliyoiwasilisha bungeni hivi karibuni ya mwaka wa fedha 2018- 2019 .

Aidha amesema ujenzi huo wa vituo saba vya umahiri vitagharimu zaidi ya shilingi bilioni 11 na kuongeza kuwa serikali imetoa kandarasi kwa kampuni ya suma jkt kwasababu yauwezo wao wakiufundi na utekelezaji wa kazi kwa wakati pamoja na gharama kuwa nafuu ikilinganishwa na kampuni nyingine kwani kupitia suma jkt serikali itaokoa takribani shilingi milioni mia mbili (200).

Awali akizungumza wakati wakusainishana mikataba hiyo katibu mkuu wa wizara ya madini prof, simon msanjila amesema tukio hili ni kubwa kwani vituo hivi vitatumika katika kusaidia nakuelimisha wachimbaji wadogo kuhusu bioashara ya madini

Kwaupande wake mhandisi  morgan nyonyi  mkurugebnzi mwendeshaji wa kampuni ya ujenzi ya suma jkt amesema wao kama wakandarasi wamejipanga na wamejiandaa katika kutekeleza miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati kwa muda wa miezi 6 kama mkataba unavyoelekezaGet it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.