Header Ads

YALIYOJIRI LEO JULAI 12, 2018 WAKATI WA KIKAO KATI YA WAZIRI MKUU, MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA NA MAAFISA UGANI JIJINI DODOMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekutana na Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa nchi nzima ili kujadili na kupanga mipango mbali mbali ya kuendeleza sekta hizo. 


Kikao hicho cha siku mbili kimehudhuriwa na Maafisa Ugani takriban 600 kutoka mikoa mbali mbali nchini. 


Wataalam wa Kilimo, mifugo na Uvuvi mna dhima kubwa ya kuhakikisha mnasimamia sekta hizo ili ziendelee kutoa mchango katika kuendeleza sekta ya viwanda nchini - Waziri Mkuu Majaliwa. 

Sekta za kilimo, mifugo na uvuvi haziwezi kuendelea kuchukuliwa kama sekta za kujikimu pekee bali zinatakiwa zibadilishwe kuwa za kibiashara zaidi - Waziri Mkuu Majaliwa. 

Natoa agizo kwa Maafisa Ugani kuimarisha usimamizi, uratibu, tathmini na ufuatiliaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo nchini ili ilete mafanikio makubwa - Waziri Mkuu, Majaliwa. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.