Header Ads

Askofu Pengo awaalika waumini katika mapokez ya Ruwaichi.


 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam wa Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewaalika waumini wa dhehebu hilo kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Askofu Mkuu mwandamizi, Yuda Thadeus Ruwa'ichi.
Taarifa ya Katibu wa jimbo hilo, Padri Frank Mtavangu iliyotolewa jana Jumatatu Agosti 27, 2018 inaeleza kuwa mapokezi hayo yatafanyika Ijumaa Septemba 7, 2018.
Juni 2018, Papa Francis wa 16 alimtangaza Ruwa’ichi kuwa askofu mkuu mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Padri Mtavangu amesema katika kufanikisha mapokezi hayo, “Kardinali Pengo anatualika wote kushiriki katika mapokezi haya. Askofu mkuu mwandamizi atapokelewa rasmi kijimbo kwa adhimisho la misa takatifu itakayoanza saa 10:00 jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu.”

“Mara baada ya misa kutakuwa na hafla fupi ya chakula cha jioni katika viwanja vya shule ya sekondari na msingi ya Millenium (zamani Forodhani) ambapo maklero wote na wawakilishi wa rnakundi mbalimbali watashinki.”

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.