Header Ads

BETHIDEI YA TIFFAH KUBUMA, MAMA MONDI AZUA GUMZO!Siku chache baada ya bethidei ya mjukuu wake, Latifah Nasibu ‘Tiffah’ kubuma Afrika Kusini ‘Sauz’, mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ amezua gumzo kwa kuonekana kwenye klabu ya usiku ya The Legend iliyopo Namanga jijini Dar.

Tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo, mama huyo alionekana akiwa hana wasiwasi ndani ya klabu hiyo akiburudika na mama mwingine aliyekuwa ameongozana naye ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio, alishuhudia baadhi ya mashabiki wakiacha kufuatulia burudani iliyokuwa ikipigwa na Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ wakihoji kulikoni zile mbwembwe zote alizotoa kuwa atakuwepo Sauz kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mjukuu wake.
“Si alitakiwa kuwepo Sauz huyu? Mbona anazuga tu Bongo, ama kweli zilikuwa mbwembwe kumbe hakuna lolote, hakuna cha safari wala nini, bethidei imebuma,” alisikika mtu mmoja aliyekuwa ukumbini hapo. Hata hivyo, baada ya maneno kubuma kwa bethidei kutawala kila kona, mama Diamond aliinuka na kuondoka zake akiacha gumzo karibu ukumbi mzima kumzungumzia.
Tiffah alizaliwa Agosti 6 lakini baba yake, Diamond aliamua kuisogeza sherehe hiyo ya kuzaliwa kutokana na majukumu ya kikazi, hivyo akaandaa kumfanyia sherehe kubwa kwa kushirikiana na familia yake na wadau mbalimbali, Agosti 17 huko Sauz lakini bethidei hiyo haikufanyika.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.