Header Ads

Fahamu wasanii wanao lipwa pesa ndefu duniani


Muigizaji Dwayne Johnson maarufu kama 'The Rock

Muigizaji George Clooney amefanikiwa kumtoa kileleni Dwayne Johnson maarufu kama 'The Rock' kwenye orodha ya wasanii wa kiume wanaolipwa mkwanja mrefu duniani huku mwanadada Scarlett Johannson akishika nafasi ya kwanza kwa wanawake duniani.

The Rock aliwahi kuongoza nafasi hiyo ya kwanza kwa takribani mara mbili kulingana na mapato yake kwa mwaka 2017 ambapo alikuwa anaingiza kiasi cha Dola milioni 119 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kwa mujibu wa orodha ya Jarida la kibiashara la Forbes.
Wakati jarida la kibiashara la Forbes likitoa orodha hiyo ya wasanii wanaolipwa fedha nyingi duniani kupitia kazi zao, nchi ya Tanzania bado ipo katika wakati mgumu wa kuweza kutambua thamani halisi ya msanii mmoja mmoja kutokana na watu hao kufanya mambo yao kiusiri na kudhania kwamba wakitaja viwango vyao huenda wakachekwa au kudharauliwa.
Cheki hapa chini orodha ya waigizaji 10 bora  kwa upande wa wanaume na ikifuatiwa ya wanawake kwa chini yake.
Nafasi Jina Kiwango
1. George Clooney $239m
2. Dwayne Johnson $119m
3. Robert Downey Jr $79m
4. Chris Hemsworth $64.5m
5. Jackie Chan $45.5m
6. Will Smith $42m
7. Akshay Kumar $40.5m
8. Adam Sandler $39.5m
9. Chris Evans $34m
10. Salman Khan $33.5m
Upande wa wanawake ni kama ifuatavyo:-
Nafasi Jina Kiwango
1.  Scarlett Johansson  $40.5m
2. Angelina Jolie $28m
3. Jennifer Aniston  $19.5m
4. Jennifer Lawrence  $18m
5. Reese Witherspoon  $16.5m
6. Mila Kunis $16m
7. Julia Roberts $13m
8. Cate Blanchett $12.5m
9. Melissa McCarthy $12m
10. Gal Gadot  $10m

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.