Header Ads

"Ili uwe 'star' kikamilifu hupaswi kuwa na 'skendo'' JohariMsanii mkongwe wa filamu nchini Tanzania, Blandina Chagula maarufu kama Johari amedai, anachukizwa na tabia za baadhi ya wasanii kupenda kutengeneza 'skendo' na kuacha kufanya kazi zilizokuwa bora
Johari ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya kuwepo wimbi kubwa la wasanii kupenda kutengeneza 'skendo' ili kusudi wapate unafuu katika kutoa kazi zao.
"Ili uwe 'star' kikamilifu hupaswi kuwa na 'skendo', lazima uzikimbie ili kusudi uweze kufanya kazi zako vizuri kama kioo cha jamii. Kwa hiyo mtu anavyoruhusu 'skendo' ili aweze kuzidi kukaa au ku-hit kwenye 'game', mimi naona hajijengee misingi mizuri ya jina lake na badala yake anakuwa ameliegesha tu", amesema Johari.
Pamoja na hayo, Johari ameendelea kwa kusema "sanaa haitaji 'skendo' na ili uweze kuendelea kufanya sanaa nzuri ni lazima uweke heshima na uheshimike kwa jamii ambayo wewe unaweza kuielimisha, hivyo nawaambia wafanye kazi tu na endapo watafanya hivyo sanaa zao zitawatangaza nasio skendo".
Mbali na hilo, Johari amedai haitoweza kuja kutokea maisha yake kuja kuyaweka hadharani kwa kuwa sio kila kitu kinapaswa watu wakifahamu.
Johari ni miongoni mwa wasanii waliopo nchini Tanzania walioweza kujipatia umaarufu mkubwa kupitia kazi zake pamoja na mali nyingi, lakini cha ajabu msanii huyo amekuwa msiri wa kujitangazia mafanikio aliyonayo kama wanavyofanya wenzake kwenye mitandao ya kijamii, na kumfanya kuendelea kujipatia heshima kubwa hadi leo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.