Header Ads

“Jamani yule ni mshkaji tu'' Johari

MREMBO mkongwe Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’ amedaiwa kuonja penzi la kijana wa mjini, Petit Man ambaye ni mume halali wa dada wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan.
Chanzo makini kilipenyeza kuwa wawili hao waliwahi kubanjuka kipindi cha nyuma na hata juzikati walinaswa chombingo kwenye uzinduzi wa filamu ya msanii Daud Michael ‘Duma’, Nipe Changu uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.
Baada ya kupenyezewa picha ya wawili hao wakiwa pamoja Mlimani City, Amani liliwatafuta na kufanikiwa kuzungumza na Johari huku Petit simu yake ikiita bila kupokelewa.
“Jamani yule ni mshkaji tu na tukiwa karibu watu wanadhani tunatoka, sijawahi kutoka naye na sidhani kama ninaweza kufanya hivyo sababu ni mume wa mtu, naheshimu,” alisema Johari.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.