Header Ads

klabu ya Real Madrid yawasilisha mamalamiko yake

Klabu ya Real Madrid imewasilisha malalamiko yake kwa shirikisho la kandanda duniani FIFA juu ya Inter Milan kumvizia kiungo wa klabu hiyo, Luka Modric bila klabu hiyo kupewa taarifa yoyote.
Mchezaji huyo ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi, amewekewa bei ya uhamisho yenye thamani ya Pauni 750 millioni akibakiza mkataba wa miaka miwili klabuni hapo.
Inter Milan wamelalamikiwa kufanya mazungumzo ya wazi na mchezaji huyo bila ya klabu husika, Real Madrid kuhusishwa, ambapo kocha wa Inter Milan, Luciano Spalletti aliwahi kukaririwa kuwa wako katika mpango rasmi wa kutengeneza mazingira ya kumfanya Luka Modric kujiunga na klabu hiyo.
Uthibitisho mwingine wa viongozi wa Inter kutojizuia kuzungumzia suala hilo ni kauli ya mkurugenzi wa klabu hiyo, Piero Ausilio ambaye alithibitisha klabu yake kumfukuzia mchezaji huyo kabla ya mchezo wa kirafiki wa Atletico Madrid na Inter Milan wikiendi iliyopita.
Hatua hiyo ya Real Madrid imekwenda sambamba na maoni ya viongozi wa juu wa La Liga wakiongozwa na Rais, Javier Tebas ambaye amelalamikia matumizi mabaya ya pesa ya baadhi ya klabu kubwa za ulaya ambayo hufadhiliwa na mabosi wa klabu hizo na hata Serikali.
“Tunachotakiwa kufanya ni kujiuliza sisi wenyewe kwanini haya yanatokea, tunatakiwa kujiuliza kwanini klabu ambazo zinafadhiliwa na serikali zinavuruga soko la wachezaji “, amesema Tebas.
“Nazungumzia kuhusu PSG, lakini pia Juventus kwa kumsajili Ronaldo na hata hizi ofa za Inter Milan ambao hawana pesa ya kusajili wachezaji wakubwa halafu wanatangaza ofa kubwa ya kumsajili Modric, sijui yanatokea wapi “, ameongeza.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.