Header Ads

Mechi ya Simba imesogezwa mbele

Ligi Kuu soka Tanzania Bara imeanza kutimua vumbi leo ambapo mechi sita za ufunguzi zitapigwa leo Agosti 22, ambapo mpaka sasa mechi tano zimemalizika huku Simba ikitarajiwa kushuka dimbani saa 2:00 usiku dhidi ya Prisons uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Michezo iliyomalizika ni Alliance FC dhidi ya Mbao FC ambapo Mbao imeshinda goli 1-0, Kagera Sugar ameshinda 2-1 dhidi ya Mwadui FC, Ndanda FC 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting , Bishara United ikiibika na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wake Singida Utd katika dimba la Namfua, huku Costal Union ikitoka suluhu ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli FC.
Awali mchezo wa Simba ulitangazwa kuwa utachezwa saa moja jioni katika uwanja wa Uhuru ambapo baadae Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitoa taarifa ya kusogezwa mechi ya Simba dhidi ya Prisons ambayo itachezwa saa mbili usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alithibitisha mchezo huo utachezwa saa mbili usiku na sio saa moja kama ambavyo awali ilitangazwa saa moja na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.
Simba imerejesha mechi yao Uwanja wa Taifa na kuachana na Uwanja wa Uhuru, ambapo ilitakiwa kushuka dimbani kukipiga na Prisons leo saa kumi jioni lakini mechi hiyo itachezwa saa mbili usiku katika Uwanja wa Taifa”, amesema Ndimbo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.