Header Ads

"Mimi kwanza sio mpenzi wa mitandao'' Mama kanumba


Mama wa marehemu Steven Kanumba, amefunguka na kudai hajawahi kutumia mitandaoo ya kijamii kutafuta umaarfu kama watu wasemavyo bali umaarufu unamfuata yeye kutokana na miujiza ya Mun
Mama Kanumba ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya kuenea video mitandaoni zilizokuwa zikimuonyesha akitoa maneno mbalimbali juu ya wasanii wa filamu nchini baada ya kifo cha mwanae kutokea.
"Mimi kwanza sio mpenzi wa mitandao na wala sitafuti umaarufu lakini ni maajabu ya Mungu, umaarufu unanitafuta wenyewe. Kwa hiyo wanaondelea kusema waendelee tu kwa sababu midomo hailipiwi VAT. Mimi nitaendelea kuwa mama Kanumba na kumkumbuka mwanangu",amesema Mama Kanumba.
Pamoja na hayo, mama Kanumba ameendelea kwa kusema kuwa "waone ajabu Kanumba amefariki huu ni mwaka wa saba lakini bado watu wanaendelea kumkumbuka na kumuenzi".
Mbali na hilo, mama Kanumba amesema anashukuru jinsi ambavyo waigizaji maarufu mbalimbali wanavyomkumbuka na kumualika katika matukio yanahusisha tasnia hiyo kwa niaba ya mtoto wake Steven Kanumba.
Tokea alipofariki staa filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba mnamo mwaka 2012, mama huyo amekuwa gumzo mitandoni na sehemu nyingine mbalimbali kutokana na kauli zake, zilizokuwa zinawaponda baadhi ya wasanii katika tasnia hiyo kwa kile anachokidai kila uchao suala la unafiki.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.