Header Ads

Mr Blue yupo tayari kuacha muziki kwa ajili ya familia yake

Msanii Mr Blue amefunguka na kumshukuru sana mke wake ambae ni mama wa watoto wake kuwa kuwa amekuwa moja ya watu walioweza kumbadilisha sana mpaka kufikia ambapo alipo sasa hivi , sehemu ambayo hata yeye anaona kuwa amebadilika sana.

Mr Blue anasema kuwa kutokana na mchango mkubwa wa mke wake katika kumbadilisha, hata yeye amekuwa aifikiria jinsi gani anaweza kuifanya familia yake kuwa na furaha na anaona njia moja wapo ya yeye kufanya hivyo ni kukaa na kutulia hata  ikibidi kuacha muziki ili kumrudia mungu kwa ajili ya furaha yake , mkewe na familia yake pia.

Mr blue anasema kuwa mke wake ni swala tano , kitu kinachomsukuma zaidi yeye kutaka kutoka katika muziki ili kurudi na kuanza kuswali kutokana na msukumo mkubwa wa kidini kutoka kwa mke wake.

Naomba mungu ipo siku najua nitaacha muziki kabisa na mimi nipumzike na kutulia kabisa , umri unakwenda pia,sio utani siwezi kusema ni officil lakini kama mke wangu atataka nifanye nitafanya kwa sababu nina mpenda sana. -Alisema Mr Blue alipokuwa akiongea na Bongo5.
TOA MAONI YAKO HAPA

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.