Mwandishi wa habari ahojiwa na polisi kwa matumizi mabaya ya mtandao
Mwandishi
wa habari wa gazeti la Uhuru, Constantine Mathias, amehojiwa na polisi
kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao na kujihusisha na vitendo vya
rushwa.
Akizungumza
jana Agosti 23 Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu, Deusdedit Nsimeki
alisema Mathias alikamatwa, akahojiwa kisha akaachiwa.
Imeelezwa
kuwa Mathias alisambaza picha kwenye mtandao wa kijamii wa facebook
inayomuonyesha askari polisi akinywa bia akiwa na sare za kazi.
Picha anazodaiwa kusambaza ni za askari polisi PC Neto Mahenge wa kituo cha polisi Mwamapalala.
"Anahojiwa
kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na madai ya
kujihusisha na vitendo vya rushwa. Nimeagiza achukuliwe maelezo na
kuachiwa kwa dhamana akikamilisha taratibu na mahitaji ya kisheria,"
alisema Kamanda Nsimeki.
No comments:
Post a Comment