Header Ads

Nai asema yuko tayari kuwapaka wasanii wa kiume Lipstik
Video vixen' maarufu na 'Makeup Artist' ambaye pia ni mpenzi wa rapa Moni Centrozone, Nai, amefunguka na kudai yupo tayari kuwapaka wasanii wa kiume 'lipstick' pamoja na kuwavalisha mawigi ili kusudi wawe na mvuto zaidi katika video zao.

Nai amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya kusambaa kwa 'video' ambayo inamuonesha rapa Country Boy akiwa amepaka rangi ya mdomo inayofanana na aliyopaka mrembo huyo.
"Sasa hivi nimeona ni bora ni 'deal' sana na wasanii wa kiume kwasababu wengi wao wamekuwa wakitokea katika video zao wakiwa simple yaani yupo natural yeye kama yeye na machunusi. Unajua wakiwa katika muonekano wa makeup wanakuwa wazuri, mwanaume akipakwa wanja chini ya macho inamfanya anapendeza zaidi", amesema Nai.
Pamoja na hayo, Nai ameendelea kwa kusema "kupaka 'lipstick' ni ubunifu. Kiukweli nina mikakati ya kuwabadilisha wasanii wa kiume bongo kwasababu wamekuwa wakitokea kawaida sana". 
Wazo hilo la Nai kuwapaka wanaume 'lipstick' pamoja na kuwavalisha mawigi limekuja takribani miezi mitano kupita tokea, msanii Dogo Janja kuonekana amevalia mavazi ya kike pamoja na kujiremba kabisa katika video yake ya 'wayu wayu'.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.