Header Ads

Nandy asema anatamani kuwa na famila Bora

Msanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’, amesema anatamani kuja kuwa na familia ya mfano wa kuigwa huku akitaja vigezo vitatu atakavyovizingatia.

Nandy anasema miongoni mwa sifa kubwa anazotamani ndani ya familia yake ni pamoja na ile ya kumcha Mungu, kutafuta pesa pamoja na kuwa na watoto wasiopungua watatu.

“Kila mmoja anatamani familia jinsi alivyojipanga mwenyewe, kwa upande wangu natamani sana familia iliyo bora, yenye hofu ya Mungu na ikipendeza nipate watoto wengi,” anasema Nady

Alisema anaamini wakati wake ukifika naye ataingia kwenye maisha ya ndoa na kutimiza malengo yake.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.