Header Ads

Nikki wa pili awaasa vijanaMsanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili amefunguka na kuitaka jamii hasa vijana, kuzingatia na kujiuliza zaidi kuhusu namna ya kuzifikia ndoto zao walizoziweka akili mwao ili kusudi waweze kuzifikia na sio kuishia kuwa wasindikizaji kwa wenzao.

Nikki wa Pili ametoa ushauri huo,  Agosti 21, 2018 kupitia ukurasa wake maalum wa kijamii wa Instagram baada ya kuwepo wimbi kubwa la vijana kuwa na ndoto mbalimbali lakini wanashindwa kuzifikia kutokana na sababu mbalimbali ambapo ikiwemo na wao wenyewe kufikiria namna ya kujipanga kufika wanapohitaji.

"Toka nimeiweka wazi ndoto yangu ya kuwa rais, maswali yamekua mengi sana. Ningependa maswali kama hayo pia mjiulize nanyi juu ya ndoto zenu, ili nitakapokuwa rais niwe na taifa la watu wanaoelewa ndoto zao ambapo itakuwa rahisi kwangu kuwasaidia kuzifikia", ameandika Nikki.

Pamoja na hayo, Nikki ameendelea kwa kusema "ila kama mnauliza sana juu ya ndoto yangu, nitakuja kuwa rais wa watu wasioelewa kuwa wanataka nini katika maisha yao na mwishowe mambo yatakuwa magumu".

Hii si mara ya kwanza kwa msanii Nikki wa Pili kuwaasa vijana kuchangamsha akili zao katika kufikia malengo yao waliojiwekea huko mbeleni, kwani itakumbukwa mnamo Julai 26, 2017 aliwashauri vijana waliozaliwa katika ardhi ya Tanzania kuacha kufuta mifumo au mitazamo isiyo akisi katika ujana wao na badala yake wajitume katika kupambana na hali ya maisha ili waweze kufanikiwa maisha kabla ya miaka 38.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.