Header Ads

NINJA AIWEKA KABATINI JEZI YA CANNAVARO

Abdallah Shaibu.
JEZI ya Yanga yenye namba 23 ambayo Nadir Haroub ‘Can­navaro’ alimkabidhi Abdallah Shaibu ‘Ninja’ aendelee kuitumia baada ya yeye kustaafu kucheza soka, jezi hiyo bado ipo kabatini.

Cannavaro ambaye ni meneja wa Yanga kwa sasa, hivi karibuni alitan­gaza kustaafu kucheza soka akiwa nahodha wa timu hiyo ambapo uongo­zi ulitaka kuistaafisha jezi yake, lakini yeye akakataa na kumkabidhi Ninja.
Nadir Haroub ‘Can­navaro’.
Ninja ambaye alisajiliwa na Yanga msimu uliopita, bado hajaanza kuitumia jezi hiyo na wikiendi iliyopita kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger alivaa jezi yake namba 6 aliyokabidhiwa wakati anatua Yanga.

Beki huyo ameliambia Championi kuwa, jezi hiyo anasubiri kuan­za kuitumia kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu ambao unaanza leo huku Yanga ikicheza ke­sho Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

“Unajua jezi niliyoachiwa na Cannavaro siwezi kuitumia kwenye michuano ya kimataifa kwa sababu kule natam­bulika ninaitumia jezi namba 6, lakini msimu wa ligi ukianza rasmi ndiyo nitaanza kuitumia.

“Ni jambo zuri kuo­na nimekabidhiwa jezi hii na mkongwe am­baye anaamini nitaitendea haki, hivyo nitajipanga kuhakikisha simuangushi,” alisema Ninja ambaye Ko­cha Mwinyi Zahera ameanza kumtumia kama kiungo lakini pia beki wa kulia.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.