Header Ads

Serikali imesema itahakikisha inazalisha zao la aliezeti kwa wingi
DODOMA:
Serikali pamoja na wadau wa zao la alizeti wamesema kuwa watahakikisha zao la alizeti linazalishwa kwa wingi nchi ili kufikia tani million 10 kwa lengo la kuokoa sh 400 bilion ambazo zinatumia kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi kwa mwaka.

Akizungumzia jijini hapa kwenye kikao cha wadau wa uzalishaji wa mbegu ya alizeti nchini mkulima kiongozi wa wakulima wa zao la alizeti mkoa wa Morogoro Japhet Migabo amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuhakikisha kuwa wakulima wa zao hilo wanazalisha kwa tija kama ilivyo mazao mengine.

Amesema kuwa mkulima wa kawaida akipata mbengu iliyobora na kupanda kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa uzalishaji wa aliziti nchini utaongezeka na kuweza kumaliza uagizaji wa mafuta nje ya nchini.

Naye Mkurugenzi wa maaendeleo ya mazao wizara ya kilimo Ngasebwa Chimagu  amesema kuwa ili kuongeza uzalishaji wa alizeti ni lazima wakulima wafikishiwe mbegu kwa wakati pamoja na kuacha tabia ya kupanda ilimradi ni alizeti bali wanatakiwa kupanda mbegu bora zaidi ili kuleta matokeo yanayotarajiwa.

Akizungumzia suala la sera ili kuondo tozo, Chimagu amsema wanashangaa kuona walishaondoa tozo ya usajili lakini bado kuondolewa kwa tozo hizo haziwasaidii wakulima.

Meneja masoko wa nyanda za juu kusini wa kampuni ya bytred limited waofanya kazi ya kununua mbegu ya alizeti kutoka nchini India Andew Luvanda amesema ili kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti ni vyema wakulima wakafuata taratibu hasa kipindi cha palilizi.
Amesema kuwa mazao la alizeti yanatakiwa kupaliliwa yakiwa na wiki tatu hadi nne kwa maana hiyo usipofanya palilizi kwa muda huo unaweza kupata hasara ya asilimia 15 hadi 25 katika mavuno ambayo ulipaswa kuyapata,hivyo inawekana wengi wanashindwa kupalilia kwa muda unaotakiwa na hivyo kupata mavuno kidogo.
Mwisho.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.