Header Ads

Shilole Kataja Gharama za Jumba Lake Alilolijenga Dar


Msanii wa muziki na mjasiliamali, Shilole aka Shishi ameweka wazi gharama alizotumia kujenga nyumba yake ambayo aliionyesha mtandaoni.

Akiongea na kituo cha redio cha Clouds FM jana Jumanne, Shishi amedai zaidi ya ths milioni 90 aliyoitumia imetokana na muziki wake na sio biashara zake.

“Sijawahi kukopa, nimejenga kupitia muziki wangu, hadi sasa nimetumia kama mill. 90. Ni nyumba mbili zipo kwenye uwanja mmoja,” alisema Shilole.

Aliongeza, “Mume wangu Uchebe ameikuta hii nyumba yeye alichochangia ni mawazo tu, kuhusu nyumba hii iweje,”

Muimbaji huyo amedai nyumba hiyo ameijenga taratibu taratibu kwa kipindi cha miaka 3.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.