Header Ads

“Sitafuti kiki ila nimeeleza kitu ambacho nimekuwa nakifikiria'' Sabby Angel’

BAADA ya Mtangazaji wa Redio, Loveness Malinzi ‘Diva thebawse’ kudai kuwa ana tatizo la kizazi na hivyo anahangaika kubeba mimba, staa wa Filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ameibuka na kudai kuwa yupo tayari kumbebea staa yeyote mimba ila kwa dau kuanzia milioni ishirini.

Akizungumza na Vijistori Mitandaoni, Sabby aliyewahi kudaiwa kubanjuka kimapenzi na mastaa kadhaa akiwemo Alikiba alisema kuwa, anajua kuwa wapo mastaa wa kiume walio na wapenzi wao wenye matatizo kwenye kizazi kwa hiyo yupo tayari kuwabebea mimba.

“Sitafuti kiki ila nimeeleza kitu ambacho nimekuwa nakifikiria muda mrefu baada ya kuona watu wengi wakiwemo mastaa hapa Tanzania kuwa na tatizo katika kizazi, mara mimba zinatoka na wengine kushindwa tu kubeba kwa sababu mbalimbali na ndiyo maana nikaamua kuongea hivi,” alisema Sabby na kuongeza;

“Zipo njia za kitalaamu unapandikiza mwisho wa siku unakuwa na mtoto wako ila kwangu kwa sharti moja tutasaini mkataba ambao sio chini ya milioni ishirini ili kupandikiza hizo mbegu kwa kuwa si unajua uzazi unachakaza sometimes kwa hiyo lazima nipate hela za kujitengeneza,” alimaliza Sabby

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.