Rais wa CWT Leah Ulaya, ameieleza East Africa Breakfast ya East Africa Radio kuwa kwa kushirikiana na wanasheria wao wataujadili kwa kina muswada huo ambao unapendekeza kuanzishwa kwa bodi ya walimu itakayokuwa ikisajili na kuwapa leseni walimu wote, na kutoruhusu mtu asiye na leseni kufundisha.
Tunaomba tupatiwe muda ndio tutoe maoni sahihi kwa kushirikiana na wanasheria wetu, kwa sasa hatuna majibu sahihi”,amesema Rais wa CWT.
Hayo yamejiri baada ya kuwasilishwa kwa muswada bungeni Mei 2 mwaka huu na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ambao ulipendekeza kuanzishwa bodi ya taaluma ya ualimu kama utapitishwa na kuwa sheria, mwalimu hataruhusiwa kufundisha mpaka awe na leseni.
Muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza Juni mwaka huu ambapo Spika wa Bunge, Job Ndugai, aliiagiza Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuanza kuufanyia kazi ujadiliwe katika mkutano ujao.