Header Ads

Uhamiaji Wazidi Kung’ang’ania Pasipoti ya Mkurugenzi TWAWEZA

Idara ya Uhamiaji nchini, imesema itaendelea kushikilia kwa muda usiojulikana pasi ya kusafiri ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Twaweza, Aidan Eyakuze.

Mkurugenzi huyo alinyang’anywa pasi hiyo Julai 24, mwaka huu, baada ya kuitwa na makao makuu ya idara hiyo na kutakiwa kuandika maelezo na kisha baadaye hati yake kuchukuliwa.

Msemaji wa Idara ya Uhamiaji nchini, Ally Mtanda, alisema  jana kuwa hadi sasa wanachunguza suala la uraia wake na watakapokamilisha watatoa taarifa kwa umma.

Baada ya pasi ya mkurugenzi huyo kushikiliwa, Mtanda aliwaeleza waandishi wa habari kuwa wanachunguza uraia wake na iwapo atabainika si raia atatakiwa kufuata taratibu za kuishi nchini.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.