Header Ads

VIKAO VYA BUNGE KUFANYIKA AGOST 20 HADI 31 JIJINI DODOMA

Kamati za bunge kuichambua taarifa ya CAGDar es Salaam. Vikao vya kamati za Bunge vinavyotarajia kufanyika kuanzia Agosti 20 hadi 31, 2018 jijini Dodoma vitachambua taarifa ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia Juni 30, mwaka jana.

“Kamati zinazosimamia matumizi ya fedha za umma ambazo ni Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zitachambua Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia Juni, 30, 2017,” imeeleza taarufa hiyo.
Taarifa iliyotolewa leo Agosti 17, 2018 na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano Ofisi ya Bunge imesema Spika wa Bunge, Job Ndugai, imezitaka kamati hizo kuanza shughuli zake tarehe hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 117 ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Kamati hizo zitakutana kabla ya kuanza kwa mkutano wa 12 wa Bunge Septemba 4 2018.
Taarifa hiyo imesema  shughuli zitakazofanywa  ni pamoja na kuchambua miswada mitano  ya sheria inayotarajiwa kujadiliwa na kamati nne zilizopelekewa miswada hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 84(1).
Mosi, Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa itachambua na kujadili ‘Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018.
Pili, Kamati ya Katiba na Sheria itachambua na kujadili miswada miwili ambayo ni ‘Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2018’ na ‘Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2018’
Tatu, Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii itachambua na kujadili ‘Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu Tanzania wa Mwaka
Nne, Kamati ya Bajeti itachambua na Kujadili ‘Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018’
Taarifa hiyo imesema, kamati tisa, zitapokea taarifa mbalimbali za wizara na taasisi.
Kamati ya Bajeti na Kamati ya Masuala ya Ukimwi zitachambua taarifa za taasisi/ wizara za Serikali kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwa mujibu wa Kifungu cha 7(1), kifungu cha 7(2) (i) (ii) (iii) na (iv) na Kifungu cha 9(a) vya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge.
Imesema Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo itachambua Sheria Ndogo 121 zilizowasilishwa Bungeni tarehe 9 Aprili, 2018, wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge. Madhumuni ni kutekeleza majukumu yake yalioainishwa katika Kifungu cha 11 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge.
Taarifa hiyo imesema Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) itachambua Taarifa ya Uwekezaji wa taasisi/mashirika kumi na tatu (13) kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.