Header Ads

Wakina mama washauriwa kuwahi kliniki wanapo hisi wanaujauzito

DODOMA:
Akina Mama wajawazito nchini wametakiwa  kuwahi kliniki mara wanapohisi wana ujauzito na kufuata ushauri wa watalamu wa afya  ili kuwakinga watoto wanaotarajia kujifungua dhidi ya maabukizi ya Virus vya UKIMWI.

Akizungumza   jijini Dodoma Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na  Watoto Dkt.Leonard Subi  amesema kuwa  serikali inasisitiza kuwa inataka  watoto wote nchini kuzaliwa bila virusi vya ukimwi endapo mama mjamzito ni muathirika kwa kuzingatia huduma za uzazi na afya.

''Tunataka watoto wote wazaliwe bila maambukizi ya virusi vya ukimwi, kwahiyo kama mama ameambukizwa tutumie njia ya kuweza kumpatia mama huduma stahiki ili amkinge mtoto wake '' Alisema Dk subi

Amesema kuwa tatizo la ugonjwa wa ukimwi nchini bado ni kubwa lakini wamejitahidi kupunguza maambukizi hayo na kupiga hatua kubwa baada ya kutoa elimu kwa wajawazito na jamii kwa ujumla.


Aidha amewataka wanaume kushiriki katika zoezi la kupima virusi vya ukimwi na wenza wao na siyo kuwachia wakina mama katika zoezi hilo na huduma ya mama na mtoto inapatikana katika sehemu zote nchini mijini na vijijini na kuna vituo zaidi ya elfu sita.

Pia amesema ushiriki kwa wanaume,wanawake,viongozi wa kimila na dini ni muhimu ili kuelimisha jamii kuchukua hatua ya kupima, kuhudhuria clinik na anaegundulika na maambukizi virusi vya ukimwi aendelee kutumia dawa.

Alisisitiza kuwa vituo vya kutolea huduma za afya vyote nchini hivi sasa vinatoa huduma ya elimu bure kuhusiana na afya ya uzazi na endapo mama mjamzito atagundulika ana maambukizi ya VVU ataanzishiwa dawa ambazo zitamkinga mtoto asizaliwe na maambukizi ya  Virus vya UKIMWI


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.