Header Ads

Wema awapa makavu wanaomfuatilia
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu amewataka watu wanaomchokonoa na kumfatilia mambo yake waache mara moja.

Muigizaji huyo hakuweka wazi mara moja ni nani anayemchokoza lakini mashabiki katika mitandao ya kijamii wamelihusisha suala hilo na Hamisa Mobetto, Zari pamoja sakata ambalo linadaiwa kusambaa katika mitandao ya kijamii kwamba amepata mpenzi mpya.

“Mnaniona nimekaa kimya mnanichokonoa eeh…. Mtahangaika sana wallahy…. 😒😒😒…. Niacheni tafadhal….,” aliandika Wema.

Muigizaji huyo alikuwa kimya kwa muda mrefu toka ahukumiwe na mahakama ya Kisutu kwa kosa la kutumia dawa za kulevya.

Toka tukio hilo litokee mrembo huyo amekuwa haonekanai mara kwa mara kwenye matukio tofauti na kipindi cha nyuma.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.