Header Ads

Ajinyonga baada kuwauwa watoto wake na kumjeruhu mke wake kwa pangaMTU mmoja aliyetambulika kwa jina la Donatus Isaya (35) mkazi wa Chalinze mkoa wa Pwani amejinyonga baada ya kuwauwa watoto wake wawili na kumjeruhi mkewake kwa panga.

Kwamujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, kamishna msaidizi wa polisi (ÀCP), Pudensiana Protas aliyekwenda kwenye eneo la tukio. Alisema tukio hilo lilitokea jana usiku majira ya saa tano na nusu mtaa wa Nambambo,mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea.

Kamanda Protas aliserma Donatus ambaye baada ya kutekeleza uhalifu huo wa kutisha alijinyonga aliwakatakata kwa panga wanawe wawili wa kike Grace Donatus(5) na Eriety Donatus (3) baada ya kumshambulia na kumjeruhi mkewake, Mariam Lucas ambaye alifanikiwa kukumbia na kuokoka na kifo.

Protas ambaye hakuingia kwa undani zaidi kueleza sababu zilizosababisha Donatus atekeleze unyama huo na kufanya uamuzi mgumu wa kujinyonga.Alisema miili ya watoto hao imezikwa leo.Wakati mwili wa Donatus bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea wakisubiriwa ndugu wa marehemu.Huku taratibu za kuwasiliana nao zikiendelea kufanyika.

Kuhusu hali ya Mariam, Kamanda huyo wa polisi wa mkoa wa Lindi alisema alipoteza fahamu kutokana na  kupoteza damu nyingi hasa kichwani ambako alikatwakatwa sana.Nakwamba anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Nachingwea ambako amelazwa.
Mmoja wa ndugu wa Mariam ambae alijitambulisha kwa jina la Said Mikidadi, akizungumzia tukio hilo alisema Mariam na hayati Donatus walikuwa ni wanandoa ambao walikuwa wanaishi Chanika, Dar es Salaam. Hata hivyo ndoa hiyo iliingia kwenye mgogoro uliosababisha Mariam pamoja na wanawe hao kurudi nyumbani kwake Nachingwea.

 "Wiki mbili zilizopita alikuja na kuondoka.Kwamadai kwamba alikuja kuwaona watoto wake.Hata hivyo jana alionekana wakati wa tukio tu.Haileweki alikuja lini na alifikia wapi,"alisema Said.

 Ndugu huyo wa Mariam alisema tukio hilo lilitokea saa tano na nusu wakati Mariamu akienda kulala kwenye chumba chake kilicho mlango wa nje.Ndipo alipovamiwa na kucharangwa kwa panga.Kabla ya Mariam kufanikiwa kuchomkoka mikononi mwa Donatus na kuanza kupiga mayowe akisaidiana na mama yake mzazi.

Said aliendelea kuanika ukweli  kwa  Muungwana(Jina la blogi hii)kwamba baada ya kubaini asingefanikiwa kumuuwa Mariam,Donatus aliingia kwenye chumba ambacho watoto wake walikuwa wamelala kwenye kitanda kimoja na watoto wengine wawili.

"Kwenye kitanda hicho walilala watoto wanne,yeye aliwakatakata wanawe tu.Baada ya kuhakikisha amefanikiwa kuwauwa alikwenda kwenye chumba anacholala shangazi(Mariam) ambako alijinyonga kwa kutumia kamba,"alisema Saidi.

Licha ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi na Said kuthibitisha na kueleza tukio hilo.Lakini pia mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo,ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Nachingwea,Rukia Muwango alithibitisha pia.Huku akiweka wazi kwamba alikwenda kwenye eneo la tukio na hosipitali alikolazwa Mariam.

Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Nachingwea,Dr Elias Zephanga alikiri kwamba walipokea maiti tatu na majeruhi mmoja ambae anaendelea kutibiwa na hali yake inaendelea vizuri.Akiongeza kusema Mariam alikatwatwa zaidi kichwani.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.