Header Ads

Apooza mwili baada ya kupigwa na shoti ya umeme


Mtoto Zena Aloo Rweyemamu mwenye Umri wa Miaka 6 Mkazi wa mtaa wa Tambaza Muhimbili jijini Dar es salaam , anahitaji Msaada wa hali na Mali kutoka kwa jamii baada ya kupooza mwili mzima kutokana na kupigwa shoti ya Umeme na kumsababishia Matatizo ya kupooza mwili wote na kushindwa kuzungumza.

Bibi wa Mtoto huyo bi,Lucy Moses akizungumza na Muungwan blog amesema Mtoto huyo alipatwa na tatizo hilo wakati akicheza katika makazi yao ambapo alishika bomba la Antena ambalo linadaiwa kuwa na Umeme, baada ya kushika alinaswa na kuokolewa na majirani wakati bibi yake akiwa kazini.

Aidha Bibi Lucy pamoja na Msaada wa awali aliopata kutoka kwa wananchi na majiran,i amesikitishwa na Mwenendo wa Upande uliosababisha tukio hilo ambalo walikubali kutoa kiasi cha fedha kwa ajili ya matibabu na pango lakini jambo hilo limekuwa likisuasua na kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na Rais Magufuli kumsaidia.

M/kiti wa Serikali ya Mtaa pamoja na Mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo wamekiri kuwa hali ya Mtoto zena bado ni mbaya kutokana tatizo la kunaswa na Umeme na anahitaji msaada

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.