Header Ads

Bob Junior Ajigamba kuwa Bingwa wa Kuhobga
Msanii na muandaaji wa muziki wa bongo fleva nchini, Bob Junior amefunguka na kujigamba kuwa yeye ni bingwa wa kuhonga wanawake pesa huku akidai kufanya hivyo sio ujinga bali ndio mapenzi jinsi yanavyotaka
Bob Junior amebainisha hayo kupitia ukurasa wake rasmi wa kijamii wa Instagram mchana wa leo Septemba 30, 2018 ambapo ameweka 'video clip' fupi iliyokuwa ikimuonyesha anamtunza mwanamke aliyekuwa akicheza wimbo kwa kukatika kiuno.
"Sioni shida ya kuhonga mwanamke ninaye mpenda, kumpa mwanamke pesa, gari au nyumba ni mapenzi ya kweli nasio 'ufala', kama hamjui kuhonga mtaibiwa sana. Jipange honga, muhudumie sana mwanamke wako ipasavyo ndio atulie, sio unategemea ndizi tu.. utakimbiwa shauri yako endeleni kuwa vibenten mjini mwisho wake mtaibika", amesema Bob Junior.
Katika miaka ya hivi karibuni, wanaume wengi wamekuwa wakitumia pesa zao kama fimbo ya kuwachapia wanyonge wasio kuwa na pesa, hasa hasa kwenye mapenzi na kuiba wake au wapenzi wa watu kwa kile wanachokidai kuwa pesa ndio sabuni ya roho.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.