Header Ads

"Hatuwezi kuacha watu wakaendelea kuchimba mchanga huku wakiharibu mazingira-ChongoloMkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo, Jana amefanya ziara katika eneo la Tegeta ambapo amebaini uchafuzi wa mto Tegeta na kuagiza mamlaka zinazohusika kumpa taarifa ya kina juu ya uchafuzi huo.

Chongolo alifika Salasala ambapo ni miongoni mwa Tegeta na kusema uharibifu ni mkubwa uliotokana na shughuli za kibinadamu, ikiwemo Uchimbaji wa mchanga,  jambo ambalo ni hatari kwa wananchi waliopo kandokando ya mto huo.

Baada ya kujionea uharibifu huo, mkuu huyo wa wilaya ameutaka Uongozi wa bonde la mto Wami na Ruvu ambao ndio unahusika na kutunza mazingira ya mto Tegeta kumpa taarifa ya kina juu ya uchafuzi huo.

"Hatuwezi kuacha watu wakaendelea kuchimba mchanga huku wakiharibu mazingira na baadae serikali kuingia gharama ya kuhudumia wananchi walioathirika na mafuriko wakati shughuli za uchimbaji mchanga walizifanya wenyewe" alisema.

Pia amesisitiza haiwezekani vyombo vya kusimamia vipo lakini bado mazingira yanaharibika huku akiwataka wananchi kuheshimu sheria na kulinda mito pamoja na mabonde.

Chongolo ambaye ametokea wilaya ya Longido akichukua nafasi ya Ally Hapi ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa, amebainisha kuwa hivi karibuni atafanya oparesheni ambayo itahakikisha wale wote wanaovunja sheria hawatabaki salama

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.