Header Ads

Hawa waarabu hawasikii lolote kwa Msuva, wamgomea kurudi Bongo


KIUNGO mshambuliaji wa Difaa El Jadida na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Simon Msuva, juzi Jumapili alilazimika kubakia nchini Uganda baada ya klabu yake kumzuia kutorudi nchini na wenzake wakiwa na hofu ya kuchelewa kuungana na klabu yake kambini mapema.

Msuva alikuwa sehemu ya kikosi cha Stars ambacho kilichocheza na Uganda ‘The Cranes’ juzi kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) na kumalizika kwa suluhu.

Kiungo huyo ambaye amekuwa na msaada mkubwa kwenye klabu yake ya Difaa, ameliambia Championi Jumatatu, kuwa alizuiwa na klabu yake kurejea Dar na wenzake wa Stars ambao waliondoka Uganda kutokana na kuhofia kwamba ratiba yake ingeingia mambo mengine wakati wanamhitaji kwa ajili ya mchezo wao wa wikiendi hii.

 “Nimebaki huku Uganda na kesho (leo) asubuhi nitaondoka moja kwa moja kuelekea Morocco ikiwa ni baada ya uongozi wa klabu yangu kusema kwamba nibakie hapa ili niwahi mechi ya wiki hii.

“Walihofia kwamba naweza kwenda huko Dar kisha mambo mengine yakajitokeza na kufanya nichelewe kutua kikosini kwa wakati ambapo kuna mechi muhimu wikiendi hii,” alisema Msuva.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.