Header Ads

Lungi amwaga povu kwa gigy money kisa zari kisa ni hikiMuigizaji mkongwe wa Bongo movie Lungi Maulanga amemwagia povu zito msanii wa Bongo fleva Lungi Maulanga kisa Mzazi mwenza wa Diamond Platnumz, Zari The Bosslady.

Lungi ameibuka na kudai hakufurahishwa na maneno yaliyotolewa na Gigy Money na kuelekezwa kwa Zari siku chache zilizopita baada ya wawili hao kuingia kwenye majibizano ya Mtandaoni.

Kwenye Interview yake na gazeti la Ijumaa, Lungi alisema amekuwa akikerwa mno na Gigy ambaye amekuwa akitoa kauli ya kuwa yeye ni mzuri na mrembo kuliko Zari, jambo ambalo siyo kweli kwani msanii huyo hawezi kumfikia hata robo mwanamama huyo ambaye ni raia wa Uganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini.

Huyo Gigy alipata jina kwa kukaa utupu, lakini Zari ni mwanamke mpambanaji na ana pesa zake siyo anadanga, sasa namshangaa huyo mtoto kujilinganisha naye.

Ni bora hata mimi nikajilinganisha naye kwa sababu hapa nina watoto wanne, lakini bado ninaonekana mrembo.

Sina hata tumbo, lakini yeye mtoto mmoja tu utadhani anao zaidi ya watano, namsihi anyamaze na aache kutafuta kiki kupitia jina la Zari maana siyo levo zake”.

Gigy Money alimwagia povu zito Zari mara baada ya kutoa kaulia ambayo mwenyewe aliamini ilikuwa imelenga kumdhalilisha.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.