Header Ads

Makonda Aahidiwa Sh Billion 5 na mwenyekiti wa IPP


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika mkakati wake wa kuwapa tumaini jipya watu wenye ulemavu jana ameahidiwa Kiasi cha Shilingi Billion 5 na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dk Reginald Mengi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kitakachowaajiri watu wenye ulemavu ambao wana ujuzi wa aina mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kueleza mpango wa kuwasiliana na wizara ya ardhi ombi la kupatiwa eneo la kujenga kiwanda cha kuajiri watu wenye ulemavu jambo lililomgusa Dk Mengi na kuahidi kutoa shilingi billion 5 kuunga mkono mpango huo.

Hayo yote yamejiri leo wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya kusaidia walemavu ya Dk Reginald Mengi persons with disabilities Foundation iliyozinduliwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa ambae pia amemsifu RC Makonda kwa agizo alilotoa kwa wenye viwanda kuwapa ajira walemavu kwa mujibu wa sheria na pia kampeni ya miguu bandia inayoendelea kuwasaidia walemavu.

Aidha RC Makonda pia ameeleza Mkakati wa kukutana na wamiliki wa shule binafsi kwaajili ya kuwaomba kusomesha watoto wawili wenye ulemavu bure kwa kila shule kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari ili kuwawezesha walemavu kupata elimu bora

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.